KATIBU MKUU AITAKA TIRDO NA WADAU WA VIWANDA KUTOA MAZINGIRA RAFIKI KWA WABUNIFU

::::::::::

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Balozi Waziri Rajab Salum, amezitaka taasisi zinazosimamia biashara na viwanda nchini kuwasaidia wajasiriamali wabunifu kupata mitaji ya kifedha na kuwawekea mazingira rafiki ya kiutendaji ili waweze kuanzisha na kuendesha viwanda na biashara bila vikwazo.

Akizungumza Februari 19, jijini Dar es Salaam, wakati alipotembelea Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO), Balozi Salum amesema ni heshima kwa taasisi hizo kuonekana kuwa chanzo cha ubunifu na maendeleo ya viwanda hapa nchini.

Amesema taasisi hizo zinapaswa kuwa daraja la mafanikio kwa wabunifu na wajasiriamali badala ya kuwa kikwazo katika hatua za awali za kuanzisha miradi yao.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa TIRDO, Mkumbukwa Madundo, amesema ataweka mikakati madhubuti kuhakikisha Watanzania wanafahamu shughuli na huduma zinazotolewa na shirika hilo.

Amesisitiza kuwa lengo ni kuwahamasisha vijana kujituma na kujiajiri kupitia ubunifu, ili waweze kutambulika na jamii pamoja na kutumia ipasavyo huduma zinazotolewa na TIRDO.











0/Post a Comment/Comments