
Kaimu Naibu Kamishna wa Huduma kutoka Idara ya Walipakodi wakubwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rosemary Ruganuza leo 04.02.2026 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa IDRAS kwa walipakodi wakubwa.
.......
Mfumo wa Usimamizi wa Kodi za Ndani (IDRAS) utasaidia kuboresha utoaji wa huduma, kuongeza ufanisi wa kazi na kutumia teknolojia ya kisasa katika kusimamia kodi za ndani.
Hayo yameelezwa na Kaimu Naibu Kamishna wa Huduma kutoka Idara ya Walipakodi wakubwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Bi. Rosemary Ruganuza leo 04.02.2026 Jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa mafunzo ya mfumo wa IDRAS kwa walipakodi wakubwa.
Bi. Ruganuza amesema lengo la kuwa na mfumo huo ni kuhakikisha muda mwingi wa watumishi unatumika kutekeleza majukumu ya msingi kwa ufanisi.
Ameeleza mfumo wa IDRAS utawezesha utoaji wa huduma zote za usimamizi wa kodi za ndani kwa njia ya kidijitali, jambo litakalorahisisha mawasiliano kati ya TRA na walipakodi pamoja na kuongeza uwazi na uwajibikaji.
“Tunataka muda wetu mwingi utumike katika kutekeleza majukumu yetu kwa ufanisi ili mlipakodi asipate usumbufu wowote wakati wa kupata huduma zetu," amesisitiza Bi. Ruganuza
Vile vile amesema mfumo huo wa IDRAS utatusaidia kutoa huduma bora kwa kutumia teknolojia jambo ambalo litarahisisha mlipakodi kutumia mfumo bila kufika ofisi za TRA.
Ameongeza kuwa kupitia IDRAS, walipakodi watanufaika na huduma zilizo rahisi, haraka na salama, huku Mamlaka ikiimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa usahihi na ufanisi zaidi.

Post a Comment