Hayo yameelezwa leo Februari 2, 2026 na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Mboni Mhita wakati akitambulishwa mkandarasi kampuni ya Derm Group Ltd atakayetekeleza mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vitongoji 581 kwa gharama ya shilingi bilioni 60.9 mkoani Shinyanga.
"Nimeelezwa kuwa, mradi wa HEP 2B unakwenda kuunganisha wateja wapatao 20,421. Hii inakwenda kuchochea maendeleo ya wakazi wa mkoa huu kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kufungua Viwanda na Biashara, " Amesema RC Mhita
Halikadhalika, RC Mhita amemtaka mkandarasi kuhakikisha anamaliza mradi huo wa kupeleka umeme kwenye vitongoji kwa muda uliopangwa ili wananchi wa mkoa huo waweze kunufaika na mradi ikiwemo kufungua shughuli za kibiashara.
Naye, Msimamizi wa Miradi ya REA Kanda ya Magharibi Mhandisi Robert Dulle ameeleza kuwa, kwa mkoa wa Shinyanga jumla una vijiji 509 ambavyo vyote vina huduma ya umeme, vitongoji vyenye umeme ni 2,704 na ambavyo havina umeme ni vitongoji vyenye 1,205.
Aidha, Mha. Dulle ameongeza kuwa katika mradi wa HEP 2B unakwenda kufikisha umeme kwenye vitongoji 581 kwa gharama ya shilingi bilioni 60.9 na vitakavyosalia ni vitongoji 918 tu.
Kwa upande wake, Meneja wa Kampuni ya Derm Group (T) Ltd, Mhandisi Musa Abdallah ameishukuru Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA), kwa kupewa fursa ya kutekeleza mradi huo mkoani humo. Amihakikishia Serikali kuwa mradi huo utataekelezwa kwa wakati kama ilivyopangwa kwenye mkataba na mradi unakwenda kuwa nyenzo ya uchumi katika mkoa huo.
Mwisho.





Post a Comment