Jeshi la Polisi nchini Tanzania limesema picha Mjongeo inayosambazwa kwenye Mitandao mbalimbali ya Kijamii si za matukio ya hivi karibuni bali ni tukio lililotokea Mkoani Dodoma mwaka 2023.
Taarifa kwa Vyombo vya habari iliyotolewa leo Jumapili Februari 22, 2026 na Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania Naibu Kamishna wa Polisi DCP David Misime imesema tayari Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine imechukua hatua stahiki kwa kila mmoja kwenye video hiyo kwa alivyokiuka sheria, kanuni na taratibu za nchi.
Polisi pia imetoa wito kwa wananchi kuacha kutumia au kusambaza picha za matukio yaliyopita na kuwaaminisha wananchi kuwa ni tukio la hivi karibuni, likisisitiza kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote watakaobainika kufanya hivyo vyenye kuleta taharuki kwa jamii.


Post a Comment