******
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo, amewataka watumishi wanawake wa hospitali hiyo kujitoa kwa hali na mali katika utoaji wa huduma kwa wananchi wanaofika kupiga matibabu.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani iliyofanyika leo Machi 18, 2026 katika taasisi hiyo, amesema wanawake ni nguzo muhimu katika kuhakikisha huduma bora zinatolewa kwa ufanisi, sambamba na kuchangia kufanikisha malengo ya Dira ya Maendeleo 2050.
“Wanawake tuna nafasi kubwa sana katika sekta ya afya; kujitoa kwenu kwa weledi na mshikamano ni msingi muhimu wa kuboresha huduma kwa wananchi na kufikia maendeleo endelevu ya taifa letu.” Amesema Dkt. Kimambo
Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hufanyika kila mwaka tarehe 8 Machi, yakilenga kutambua mchango wa wanawake katika nyanja mbalimbali za maendeleo pamoja na kuhamasisha usawa wa kijinsia.
Kaulimbiu ya mwaka huu inasisitiza umuhimu wa uwezeshaji wa wanawake na wasichana ili kuleta mabadiliko chanya katika jamii, ikihimiza taasisi na jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawake wanapata fursa sawa katika ajira, uongozi na maendeleo.










Post a Comment