SERIKALI YATENGA TZS. BILLIONI 200 KUWEZESHA WAHITIMU MAHIRI WA VETA KUPATA MIKOPO NAFUU.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe Prof. Adolf Mkenda (mb) akifafanua jambo mbele ya mkutano wa wasilisho la Benki Kuu ya Tanzania la kuwezesha Vijana kupata mkopo nafuu wa TZS. 200 kuendeleza ujuzi, tarehe 11 Machi 2026 - Jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Wanu Hafidh Ameir (mb) akisikiliza wasilisho la Benki Kuu ya Tanzania la kuwezesha Vijana kupata mkopo nafuu wa TZS. 200 kuendeleza ujuzi, tarehe 11 Machi 2026 - Jijini Dodoma.

.............

Dodoma. 

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia (WyEST) imepokea wasilisho kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kuhusu programu maalum ya kuwawezesha wahitimu wa mafunzo ya Mamlaka ya Elimu ya ufundi stadi (VETA) kupata mikopo kwa ajili ya kuendeleza biashara walizoanzisha baada ya kuhitimu.

Akiwasilisha taarifa hiyo jijini Dodoma Machi 11, 2026, mwakilishi wa Benki Kuu, Dkt. Martin Geniune, amesema Serikali imetenga shilingi bilioni 200 kwa ajili ya kuwawezesha vijana wenye ujuzi waliopata mafunzo katika vyuo vya VETA.

Dkt. Geniune alieleza kuwa programu hiyo haitahusu tu utoaji wa mikopo, bali pia itawasaidia vijana kuandaa mawazo ya biashara, kuandika mpango wa biashara (business plan) na kukamilisha taratibu muhimu za kupata mkopo.

Kwa upande wake, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda (mb), ameipongeza Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuanzisha mpango huo akisema kuwa utasaidia kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

Amesema mpango huo unaendana na mkakati wa Serikali wa kuunganisha vyuo na viwanda, kwa lengo la kuwawezesha wahitimu kutumia ujuzi wa vitendo kujiajiri na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.





0/Post a Comment/Comments