Na Mwandishi Wetu, Dodoma.
Baadhi ya wakulimw na Wanufaika wa mradi wa mashamba ya Serikali ya Jenga kesho iliyobora(BBT)wapatao 300 katika Kijiji cha Mlazo kata Ndogowe Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma wamepatiwa Semina ya kufahamu changamoto ya Afya ya Akili,Afya ya Uzazi na namna ya kujinginga na magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya Ngono
Msomaji Lusinde na Sharifa Athuman Isaka miongoni kwa vijana na wananchi wa Ndogowe wamesema kuwa Semina hiyo imewajengea Imani,matumaini,uvumilivu na uhakikika wa upatikanaji wa mazao kupitia shughuli zao za kilimo biashara
Wameongeza kwa kusema kuwa hapo awali walikuwa hawana uelewa kuhusu chanagamoto ya Afya ya Akili na Afya ya Uzazi ambapo wameahidi kutumia elimu waliyoipata kupitia semina hiyo kuongeza nguvu katika shughuli zao za kilimo biashara
Kwa upande wake Afisa Mtendaji wa kijiji Cha Mlazo Bi. Mahawi Makasi amesema kuwa katika eneo hilo hawajawahi kupatiwa semina ya namna hiyo hivyo Serikali kupitia BBT imefanya jambo jema ambapo pia ameomba Semina hiyo iwe endelevu







Post a Comment