ASASI ZA KIRAIA WAHIMIZA ADHABU ZA VIBOKO KUKOMESHWA

Mwenyekiti wa muungano wa Asasi za kiraia ambaye ni Mkurugenzi wa Nchi wa Save the Children Tanzania Bi. Angela Kauleni akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo tar 29/4/2026 kuhusu maadhimisha Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko,ambayo inayoadhimishwa duniani tarehe 30 Aprili ya kila mwaka
Mratibu wa Program tathmini na ufuatiliaji kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) Iren Ernest akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo tar 29/4/2026 kuhusu maadhimisha Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko,ambayo inayoadhimishwa duniani tarehe 30 Aprili ya kila mwaka
Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto UNICEF Tanzania,Miranda Armstrong akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo tar 29/4/2026 kuhusu maadhimisha Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko,ambayo inayoadhimishwa duniani tarehe 30 Aprili ya kila mwaka
Mkurugenzi wa uwezeshaji elimu kwa umma na ufuatiliaji haki za binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Wakili Deogratius Bwire akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam leo tar 29/4/2026 kuhusu maadhimisha Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko,ambayo inayoadhimishwa duniani tarehe 30 Aprili ya kila mwaka (na Mussa Khalid)

...................

Mashirika ya haki za watoto na washirika wa asasi za kiraia wametoa wito wa pamoja wa kuchukuliwa hatua za haraka kukomesha adhabu za viboko na kulinda watoto dhidi ya aina zote za ukatili katika mazingira ya kujifunzia.

Hayo yamejiri jijini Dar es salaam wakati Tanzania ikiadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kukomesha Adhabu za Viboko,ambayo inayoadhimishwa duniani tarehe 30 Aprili ya kila mwaka

Akizungumza Mwenyekiti wa muungano huo, Mkurugenzi wa Nchi wa Save the Children Tanzania Bi. Angela Kauleni amesema kuwa ni vyema kuzikomesha adhabu za viboko kwani zinadhoofisha utu wa mtoto na uwezo wake wa kujifunza na kufanikiwa.

“Duniani kote, karibu watoto watatu kati ya wanne wenye umri wa miaka 2–14 hupitia nidhamuya ukatili majumbani. Nchini Tanzania, zaidi ya asilimia 70 ya watoto hupitia ukatili wa kimwilikatika utoto wao, huku walimu wakiwa miongoni mwa wahusika wanaoripotiwa mara nyingikatika mazingira ya shule. Tafiti zinaonyesha kuwa adhabu za viboko husababisha hofu,kujitenga, kupungua kwa ushiriki, kushuka kwa ufaulu wa masomo, pamoja na madhara ya muda mrefu ya kihisia na kisaikolojia”amesema Kaulen

Kwa upande wake Mratibu wa Program tathmini na ufuatiliaji kutoka Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto Iren Ernest amesisitiza kuwa adhabu hizo hazinabudi kufutwa,huku Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto UNICEF Tanzania,Miranda Armstrong,akisema Ukatili hauna nafasi katika elimu kwani adhabu za viboko zinaumiza watoto na haziboresha nidhamu.

Aidha Afisa Mawasiliano kutoka Jukwaa la Watoto Zanzibar (ZCRF) Msafiri Yahaya pamoja na Mkurugenzi wa uwezeshaji elimu kwa umma na ufuatiliaji haki za binadamu kutoka Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Wakili Deogratius Bwire wameiomba serikali na viongozi wa dini kuwa sehemu ya kukomesha adhabu zinazotweza utu wa mtoto.

Asasi hizo kwa pamoja wametoa wito wa Kuchukua Hatua Kukomesha adhabu za viboko kunahitaji uongozi ulioratibiwa na dhamira endelevu. Kikundi ikiwemo kwa Watunga sera kurekebisha haraka mifumo ya kisheria na kanuni ili kupiga marufuku waziwazi adhabu za viboko katika mazingira yote, kwa kuzingatia mifumo ya utekelezaji iliyo wazi, rasilimali za kutosha na uwajibikaji wa umma.

Vilevile Wizara ya Elimu kuingiza na kupanua matumizi ya nidhamu chanya kitaifa kupitia sera zilizo

wazi, mafunzo ya kina kwa walimu na ufuatiliaji endelevu,Walimu kuunda madarasa salama na jumuishi yanayoheshimu utu wa watoto na kuzingatia,kikamilifu Waraka wa Elimu Na. 24 wa mwaka 2002 unaohamasisha nidhamu isiyo ya ukatili,Wazazi na walezi kutumia mbinu za malezi chanya zinazowaongoza na kuwalinda watoto bila ukatili.

Asasi nyingine ni Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika (WiLDAF), Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO), HakiElimu, Shule Direct, Jukwaa la Haki za Mtoto Tanzania (TCRF), Msichana Initiative, FAWE Tanzania, ZAPHA+, Shirika la Msaada wa Kisheria na Haki za Binadamu la Zanzibar (ZALHO), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), na Tume ya Huduma za Kijamii ya Kikristo (CSSC)ambapo zote kwa pamoja, wameeleza kuwa adhabu za viboko bado ni miongoni mwa aina za ukatili dhidi ya watoto zilizoenea zaidi na kukubalika kijamii nchini Tanzania.

0/Post a Comment/Comments