Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri, akizungumza leo Aprili 2, 2026 jijini Dar es Salaam
*****
DAR ES SALAAM:
Kongani ya Bagamoyo imeendelea kuwa kitovu cha uwekezaji nchini baada ya kupokea maombi 48 kati ya maombi 86 yaliyowasilishwa TISEZA hadi kufikia Aprili Mosi mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TISEZA, Gilead Teri, amesema mwitikio huo unaonyesha imani kubwa ya wawekezaji katika eneo hilo.
Amesema mbali na Bagamoyo, kongani ya Kwale imepokea miradi 20, huku Nala na Buzwagi zikibaki na miradi miwili kila moja.
Kwa mujibu wa Teri, mafanikio hayo yanachangiwa na uwepo wa miundombinu bora pamoja na sera rafiki za uwekezaji zinazotekelezwa na Serikali.
Amebainisha kuwa mradi wa Bagamoyo Eco Maritime City umeendelea kuvutia wawekezaji wengi zaidi wanaotaka kuwekeza katika sekta mbalimbali za uzalishaji.
Katika hatua nyingine, TISEZA imesaini mikataba na kampuni tisa zitakazowekeza zaidi ya Shilingi bilioni 177 katika miradi ya viwanda na huduma.
Amesema uwekezaji huo unatarajiwa kuongeza ajira pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.
Aidha, Teri ametoa wito kwa wawekezaji wa ndani kutumia fursa zilizopo kwa kusajili miradi yao kupitia TISEZA ili kunufaika na vivutio vya Serikali.










Post a Comment