MWENYEKITI wa Shirika lisilo la kiserikali la Kagera Development Foundation (KADEFO), Balozi Liberata Mulamula amewakaribisha wanakagera wote waishio mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, kushiriki jumuiko la kawaida la mkutano wa mwaka litakalofanyika Mei 10 mwaka huu.
Akizungumzia kikao hicho, Balozi Liberata Mulamula alisema jumuiko hilo ni la kawaida la mwaka, chenye lengo la kuimarisha umoja na ushirikiano, kujadili mnaendeleo ya Mkoa wa Kagera na fursa za uwekezaji kuvutia wengi katika kuimarisha ushirikiano.
"Tunawakaribisha wanakagera wote katika kikao hicho kinachotukutanisha pamoja, kuimarisha umoja wetu na kujenga mkoa wetu. jumuiko hilo litafanyika Hekima Garden Mikocheni Kinondoni Jijini Dar es Salaam, kuanzia saa tisa alasiri ambapo Mgeni wa heshima anatarajiwa kuwa, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Balozi Dk. Bashiru Kakurwa, "alisema.
Akielezea malengo ya KADEFO, Balozi Mulamula alisema ni kudumisha umoja na mshikamano katika kuchochea maendeleo ya mkoa huo, kuhamasisha wanakagera katika kunufaika na fursa za biashara na uwekezaji wa Nchi jirani, kushirikiana na serikali kuchochea maendeleo ya mkoa huo kwa kuvutia uwekezaji.
Aidha, alisema ili kufanikisha jumuiko kila mmoja anaombwa kuchangia 50,000/- kwa ajili ya kufanikisha maandalizi na ushiriki ambapo alitaja namba ya mawasiliano ni 0742 888 800 ambayo niya Erick Rwekiza.


Post a Comment