*******
Hiki ndicho alichoandika Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Ubia nchini PPPC Bwana David Kafulila kwenye Ukura wake wa X, amekumbusha kuwa,
"Kwa kipindi cha miaka 62 mfululizo, Tanzania imekuwa mfano wa kipekee barani Afrika huu ndio muungano pekee wa mataifa mawili huru uliodumu kwa zaidi ya nusu karne.
Wakati miungano mingine kama Ethiopia–Eritrea (1952–1962), Ghana–Guinea–Mali (1958–1963), na Senegambia (1982–1989) ilivunjika mapema,
Tanzania imeendelea kusimama imara na kuonyesha mshikamano wa kipekee Duniani.
Siri ya mafanikio haya haipo tu kwenye makubaliano ya kiserikali na kisheria bali kwenye asili ya udugu wa damu, mshikamano wa kijamii, na lugha ya Kiswahili inayotufanya tuwe taifa moja.
Huu ni muungano wa watu, uliojengwa juu ya historia ya pamoja na misingi thabiti ya mshikamano wa kitamaduni.
Leo tunaposherehekea miaka 62 ya Muungano, tunawakumbuka kwa heshima kuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume, waanzilishi wa safari hii ya kipekee.
Tanzania ni ushahidi hai kwamba mshikamano wa kijamii na kitamaduni unaweza kushinda vizuizi vyote na kudumu vizazi kwa vizazi alisema Kafulila.
===

Post a Comment