MALIASILI NA UTALII KILA MCHEZO KWETU NI FAINALI

.............

Klabu ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii imeendelea kujiimarisha katika kambi ya michezo inayoendelea Mkoani Njombe huku Makocha wa timu hizo wakijigamba kushinda katika michezo yote ambayo klabu hiyo inashiriki. 

Akizungumza katika viwanja vya Shule ya Sekondari Venite, Mkoani hapo, Kocha wa timu ya Maliasili Wanaume Bw. Lusinde Yusuph Nyingi amesema kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha hivyo wachezaji wote wako imara tayari kuikabili timu yeyote itakayo kutana nayo. 

Akizungumzia Mchezo wao wa kesho dhidi ya timu Viwanda, Bw. Nyingi ametamba kuwa wataichapa kichapo cha kihistoria kama onyo kwa timu zingine. 

Bw. Nyingi ametoa wito kwa wakazi wa Njombe kujitokeza kwa Wingi kuishangilia tumu yao ya Maliasili na Utalii. 

"Wananchi wa Njomba ni wahifadhi wenzetu wa Misitu, hii ni timu yao hivyo waje kwa wingi kesho kushuhudia tunavyo chakata  Viwanda". Bw. Nyingi. 

Naye Mwalimu  wa timu ya Maliasili wanake Bi. Rehema Kapellah amebainisha kuwa, wachezaji wake wote wako vizuri na hakuna majerui hivyo kwao kwenye michezo yote ushindi ni lazima. 

"Timu imefanya mazoezi kwenye hali zote, Mvua, Jua, Baridi kali hadi kwenye upepo, imesaidia wachezaji kuwa na kasi, stamina shamba ya kufunga magili" alisema Bi. Kapellah 

Michuano ya Michezo ya Mei Mosi 2026 inatarajiwa kuanza rasmi tarehe 16 Aprili, Mkoani Njombe, huku timu mbalimbali zikiwa zimesha wasili tayari kwa kuonesheana ubabe.







 

0/Post a Comment/Comments