MALIASILI YAIBURUZA HAZINA, YAZOA MEDALI 4

** *******

Na. Sixmund Begashe, Njombe 

Timu za Maliasili Sports Club chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii, zimeendelea kuwanyanyasa wapinzani wao kwa kushinda Michezo mbalimbali ya Mei Mosi inayoendekea Mkoani Njombe. 

Timu ya Kamba Maliasili Wanaume katika kumtafuta mshindi wa kwanza kundi "A" imeiburaza vibaya timu ya Hazina kwa 2-1, mchezo ambao ulikuwa ukisubiriwa kwa hamu kubwa na washabiki wa timu hizo. 

Kwa upande wa Mchezo wa riadha, wakimbiaji wa Maliasili Bw. Elibariki Buko ameshika nafasi ya 3 katika mbio za Mita 3000 na nafasi ya 3 tena kata 800, Bi. Pily Samwel naye akishika nafasi ya 3 katika mbio 3000, huku Bi. Jehovaness Sarakikya akinyakuwa nafasi ya 3 Mita 800.

Katika mashindano hayo ya mwaka huu, Wizara ya Maliasili imeshiriki pia katika michezo ya Draft pamoja na urushaji wa Tufe.








 

0/Post a Comment/Comments