....... .
Na. Sixmund Begashe, Njombe
Timu ya mpira wa Miguu ya Wizara ya Maliasili na Utalii imetinga robo fainali katika michezo ya Mei Mosi 2026 Mkoani Njombe, baada ya kuibamiza bila huruma timu ya TPDC kwa mabao 3-1.
Katika mchuano huo mkali, timu zote mbili hadi dakika ya 90 ya kipenga cha mwamuzi zilishibana nguvu kwa kufungana 1-1 ndipo zilipo ingia kwenye matuta nakuipelekea timu ya Maliasili ifunge 2-0.
Katika hatua nyingine Club ya Michezo ya Wizara ya Maliasili na Utalii ijulikanayo kama "Maliasili Sports Club" imeshiriki kikamilifu katika Mchezo wa Mbio za Baiskeli na Mpira wa Pete.
Maliasili Sports Club yenye mashabiki lukuki kutoka Mkoa wa Njombe na viunga vyake inatarajia kuendelea kuonesha ubabe dhidi ya timu nyingine shiriki kwa lengo la kuibuka ushindi katika michezo mbalimbali.







Post a Comment