MBUZI WA JINSIA MBILI AZUA TAHARUKI GEITA

....

GEITA 

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida kwenye Manispaa ya Geita, Mkazi mmoja wa Kijiji cha Nyantorotoro "B" Catherine Kachwere, ametelekeza mbuzi wake kwa Balozi wa eneo hilo kutokana na kile alichodai kushangazwa na utata wa jinsia ya mnyama huyo.

Akizungumza na mwandishi wa habari hii, amesema alipewa mbuzi huyo kama zawadi baada ya kumtibu mgonjwa aishiye mkoani Kigoma ambapo alivyo rejea nyumbani kwake alishangaa kuona utata wa maumbile hayo.

Balozi wa eneo hilo shina namba 20 mtaa wa Nyantorotoro B, Damian Mosha, amethibitisha juu ya tukio hilo huku akieleza jinsi alivyoachiwa mbuzi huyo.

Kwa upande wake Daktari wa mifugo kutoka manispaa ya Geita, Jason Mutayaba, amesema wanyama pia huzaliwa na jinsi mbili tofauti na kwamba wakati mwingine hukosa baadhi ya viungo vya mwili kutokana na mifugo ukoo mmoja kujamiiana

Chanzo: Storm Fm
 

0/Post a Comment/Comments