SERIKALI KUBORESHA RELI YA TAZARA -KATAMBI


....
Katika kuendeleza Ushirikiano kati ya Tanzania,Zambia na China ulioanzishwa na Viongozi wa nchi hizo akiwemo Rais wa Awamu ya Kwanza na Baba wa Taifa,Mwalimu Julius Kambarage Nyerere,Kenneth David Kaunda wa Zambia na Rais wa Awamu ya kwanza wa Jamhuri ya Watu wa China,Mao Ze Dong,serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan imeingia makubaliano na China ili kuweza kujenga na kuiboresha Reli ya TAZARA iliyojengwa kutoka mwaka 1970 hadi 1975.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mheshimiwa Patrobas Katambi wakati wa Kumbukumbu ya Kuwakumbuka Wataalamu 65 wa Kichina walioshiriki Ujenzi wa Reli ya TAZARA.

Akizungumza katika eneo la makaburi lililopo katika eneo la Gongolamboto Jeshini,jijini Dar es Salaam,Waziri Katambi amesema msingi wa ushirikiano ulioanzishwa na waasisi wa nchi hizo katika Nyanja ya Uchumi,Siasa,Teknolojia na Utamaduni imeendelezwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambapo watanzania wameshuhudia miradi mbalimbali iliyojengwa na inayoendelea kujengwa ikisimamiwa na wataalamu kutoka nchi ya China.

Akizungumza katika tukio hilo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki Mheshimiwa James Millya amesema wao kama Wizara ya kisekta wanaishukuru Serikali ya China kwa kuwa na mahusiano mazuri na Serikali ya Tanzania huku akisema Tanzania inawaheshimu kwani wakati nchi ya China ikiwa aijaendelea Kipindi hicho walikuja kusaidia nchi ya Tanzania ambapo sio rasilimali fedha tu ilitumika bali hadi wataalamu mbalimbali walipoteza maisha.

Balozi wa China nchini Tanzania,Chen Mingjian amesema wao kama Serikali ya China wanaendeleza uhusiano ulioanzishwa na waasisi wa mataifa matatu ya China,Tanzania na Zambia huku akiweka wazi ushiriki wa nchi ya China katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

0/Post a Comment/Comments