Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imezindua rasmi tawi lake jipya Ubungo (EACLC), Dar es Salaam ikiwa ni hatua muhimu ya kusogeza huduma za kifedha karibu zaidi na wananchi.
Mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amesisitiza umuhimu wa sekta ya benki katika kukuza uchumi na kuwawezesha wajasiriamali, mama lishe na wafanyabiashara wadogo kupata mitaji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw. Adam Mihayo, amesema benki itaendelea kupanua huduma zake na kuwekeza zaidi katika mifumo ya kidijitali ili kuwahudumia wananchi kwa urahisi na usalama.
📊 Hadi sasa TCB ina: • Matawi 82 nchi nzima
• Mawakala zaidi ya 7,000
• Mali zenye thamani ya trilioni 2.4
📍 Tawi la Ubungo linatarajiwa kuongeza kasi ya shughuli za kiuchumi na kukuza biashara katika eneo hilo.
Karibu TCB – Pamoja Kujenga Uchumi Imara 💼✨
#TCB #Ubungo #DarEsSalaam #FinancialInclusion #Biashara #Uchumi #Tanzania

Post a Comment