
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mazingira Plus Abdalah Mikulu akizungumza katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.
Mratibu wa program kutoka Taasisi ya Mazingira Plus Fatuma Maulid akiwaelimisha vijana kujusu utengenezaji wa Mboji katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.
Afisa Maendeleo ya Jamii- United Planet Tanzania Janeth Filbert akizungumza katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam.
Mwalimu Mlezi wa Maizngira kutoka shule ya Sekondari Kibasila Emmanuel Sedekia akitoa maoni yake katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam


Mwalimu Mlezi wa Maizngira kutoka shule ya Sekondari Kibasila Emmanuel Sedekia akitoa maoni yake katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam



Baadhi ya vijana waliohudhuria katika warsha maalum ya Vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri iliyofanyika sekondari ya Kibasila Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam (picha na Mussa Khalid)
......................
Takriban Vijana 40 wakiwemo wanafunzi wa Vyuo Vikuu wahitimu,na wanafunzi wanaoendelea na masomo wamesisitizwa kutumia taka kama fursa ili kujikwamua kiuchumi.
Hayo yameelezwa leo jijini Dar es salaam katika warsha maalum kwa vijana iliyoratibiwa na Taasisi ya Mazingira Plus kwa kushirikiana na United Planet Tanzania,TCCI pamoja na Manispaa ya Temeke ambayo imefanyika katika Shule ya Sekondari Kibasila iliyopo Manispaa ya Temeke ikiwa ni katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Taka sifuri.
Akizungumza katika warsha hiyo Afisa Afya Maingira,Kitengo cha Udhibiti Taka na Usafi wa Mazingira Temeke Joseph Mpelumbe amesema kuwa elimu inayotolewa kwa vijana itawasaidia kuweza kufahamu kuchambua kata kuanzia ngazi ya kaya.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mazingira Plus Abdalah Mikulu amesema kuwa lengo lao watu waziangazie taka za kuoza kwani zinamadhara kwa kuchangia uzalishaji wa hewa ukaa zaidi ya asilimia 10.
Kwa upande wake Mratibu wa program kutoka Taasisi ya Mazingira Plus Fatuma Maulid amesema wamewafunza vijana utengenezaji wa Mboji ili kuweza kujiajiri huku Afisa Maendeleo ya Jamii- United Planet Tanzania Janeth Filbert akisema ni vyema wananchi wakawa na tabia ya kupunguza vitu vinavyopelekea uzalishaji wa taka kama chupa za Plastic
Nao baadhi ya washiriki katika warsha hiyo akiwemo Mwalimu Mlezi wa Maizngira kutoka shule ya Sekondari Kibasila Emmanuel Sedekia ameipongeza Mazingira Plus kwa kuendelea kutoa elimu kwa jamii huku baadhi ya wanafunzi wanafunzi wakisema watahakikisha wanawaelimisha wanafunzi wenzai kutumia taka kama fursa.
Maadhimisho hayo ya Kimatifa ya Taka Sifuri hufanyika Machi 30 kila Mwaka Duniani na yameenda sambamba na utoaji wa elimu ya fursa zilizopo kwenye taka huku kauli mbinu ya Mwaka huu ni Kuiwezesha Taka Sifuri katika Sekta ya Chakula.













Post a Comment