WATU 37 WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA MAKOSA YA KIMTANDAO

........

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewakamata watu 37 kwa tuhuma za makosa ya kimtandao ikiwemo kutoa vitisho na lugha za matusi mazito kwa watu mbalimbali.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es salaam,Kamanda wa Jeshi hilo Jumanne Muliro amesema watuhumiwa hao waliwakamata mnamo tar 20/04/2026 eneo la Ubungo Dar res Salaam ambapo kundi hilo baadhi yao wamebainika ni wafanyakazi wa kampuni ya INNOVIX CALL CO LTD na OTAIGO FINANCIAL SERVICES COMPANY LIMITED inayojishughulisha na ukopeshaji wa pesa kwa njia ya mtandao.

Kmanda Muliro amewataja baadhi ya watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na Renatus Mujwahuzi maarufu migeyo Mkazi wa Mbezi Beach,Odilia Oswin Maarufu ngunga Mkazi wa Goba njia nne, na Theresia Brastius maarufu kanu Mkazi wa Mtoni Kijichi na wenzao 34 ambapo hatua zaidi zinachukuliwa ili kuwafikisha kwenye

Aidha amesema kuwa Polisi Dar es Salaam ina baadhi ya takwimu za kipindi cha mwezi Machi hadi Aprili 2026 ambazo baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa na kufukishwa kwenye mifumo mingine ya kisheria.

“Watuhumiwa waliopatikana na hatia ni pamoja 1.Hashimu Kasimu @duma mkazi wa Kimara alihukumiwa na Mahakama yaWilaya ya Ubungo kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti 2. Vicent Laurent @ndimbo mkazi wa Urafiki Kinondoni alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kifungo cha maisha jela kwa kosa la kubaka 3. Habibu Nassoro mkazi Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha maisha jela kwa kosa la kulawiti 4. Ismail Ally @muro Mkazi wa Charambe alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka “amesema kamanda Muliro

Wengine ni Nelson Julius mkazi wa Mavurunza Kimara alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Ubungo kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la unyang ‘anyi wa kutumia silaha , Fadhili Issa mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka ,Peniel Jonathan @mtakibaleza mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na Yusuph Iddi mkazi wa Mbagala alihukumiwa na Mahakama ya Wilaya ya Temeke kifungo cha miaka 30 jela kwa kosa la kubaka na kumpa mimba mwanafunzi.Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali zenye viashiria vya kihalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka na kuonekna.

 Jeshi hilo limetoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali zenye viashiria vya kihalifu ili ziweze kufanyiwa kazi kwa haraka na kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili haki iweze kutendeka na kuonekna.


 

0/Post a Comment/Comments