ARSENAL YABEBA UBINGWA WA EPL BAADA YA MIAKA 22

******

Arsenal yatwaa ubingwa wa Premier League 2025/26 baada ya Manchester City kulazimishwa sare ya Goli 1-1 kutoka kwa Bournemouth, matokeo hayo yanamaanisha hakuna timu itakayoweza kufikia alama za Arsenal na zote zikiwa zimesaliwa na mchezo mmoja.

Hadi sasa Arsenal ina pointi 82, Man City ni ya pili ina alama 78 na ya tatu ni Manchester United yenye pointi 68.

Kabla ya ubingwa wa safari hii, Arsenal ilibeba ubingwa huo Mei 15, 2004 ikiwa chini ya Kocha Arsene Wenger wakati safari hii inanolewa na Mikel Arteta.

 

0/Post a Comment/Comments