B'MULO YAKUSANYA ASLIMIA 93 KABLA YA MWAKA WA BAJETI KUISHA

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Biharamulo, Innocent Mkandala

..............

Biharamulo

"UMOJA ni nguvu na utengano ni udhaifu" ndivyo unavyoweza kusema kutokana na halmashauri ya wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera kufanikiwa kukusanya mapato ya ndani kwa aslimia 93 ya lengo tarajiwa kabla ya kumalizika kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha.

Hicho ni kiashiria cha usimamizi thabiti na mifumo madhubuti ya ukusanyaji mapato ya serikali, hali inayoakisi kuchochea maendeleo ya umma hasa katika miradi ya maendeleo iliyokwama kukamilika awali.

Kutokana na hali hiyo, Baraza la madiwani wa halmashauri hiyo kwa kauli moja limempongeza Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Innocent Mkandala, kwa usimamizi mzuri na mahusiano bora kwa watumishi na watendaji wengine.

Akiongea na "Torch Media" Mkandala amesema kufikiwa lengo la makusanyo ya ndani itasaidia ku kugharamia miradi ya maendeleo kama ujenzi wa madarasa, vituo vya afya, na miundombinu ya maji.

Mbali na hilo itasaidia kuongeza uwezo wa halmashauri hiyo kutoa huduma bora na kwa wakati.

Hata hivyo makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Amelia Nyakake, amesema ushirikiano mzuri kati ya madiwani (wawakilishi wa wananchi) na watumishi (watendaji) umejenga mazingira ya uwazi na uwajibikaji.

Kwa mwaka wa fedha 2025/26, Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo ilikadiria kukusanya na kutumia jumla ya shilingi bilioni 51 huku fedha kutoka mapato ya ndani ikiwa ni shilingi bilioni 3.2






 

0/Post a Comment/Comments