...........
Na. Sixmund Begashe, Dodoma
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Chemchemi ya Jijini Dodoma, wamefanya Utalii wa ndani katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali yanayohusu uhifadhi na Utalii nchini.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa Utawa na Usimamizi wa Rasilimaliwatu, Afisa Tawala, Bw. Leodger Kiwia, ameupongeza uongozi wa shule hiyo kwa maamuzi sahihi ya kuwa na program za kiutalii na uhifadhi ambazo zinawasaidia watoto kujifunza na kurithi masuala ya Maliasili na Utalii.
Bw. Kiwia ametoa wito kwa taasisi zingine za kielemu kuwa na program za kuwatembeza wanafunzi katika maeneo ya uhifadhi na Maliasili ili wawezi kujifunza na kuburudika kupitia urithi wao adhimu wa Maliasili nchini.
Pamoja na kuupongeza na kuushukuru uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa kwa kazi nzuri ya uhifadhi na kuinua utalii, Mwalimu Mkuu Msaidizi wa Shule hiyo, Mwl. Emmanuel Msanga, amesema wataendekeea kushirikiana na Wizara hiyo kwa kuendeleza program ya kuwapeleka wanafunzi katika Hifadhi za Taifa ili kujifunza mengi kuhusu Utalii na Uhifadhi.
Naye kaka Mkuu wa Shule hiyo Breidenstein Victor, kwa niaba ya wanafunzi wenzake, amesema safari yao kwenye Ofisi za Wizara hiyo, imekuwa ya mafanikio makubwa kwa kuwa wamepata kujifunza mengi kuhusu Utalii na Uhifadhi hususani ufugaji wa nyuki wadogo wasio ng'ata.
Ziara ya shule hiyo katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii ambayo ni sehemu ya maandalizi ya safari yao ya kwenda kutalii Hifadhi ya Taifa Tarangire, ni moja ya matokeo chanya ya mkakati wa Wizara hiyo katika kuvutia watalii zaidi hususani wa ndani ili kufikia malengo ya watalii milioni 8 ifikapo mwaka 2030.








Post a Comment