................
Mkurugenzi Msaidizi wa Sehemu ya Elimu ya Afya kwa Umma kutoka Wizara ya Afya, Dkt. Rahma Hingora, ametoa elimu ya Afya kuhusu ugonjwa wa Ebola na kusisitiza umuhimu wa kuchukua hatua za kujikinga ili kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo hatari.
Elimu hiyo inakuja kufuatia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mbalimbali ya barani Afrika, ambapo kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Udhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC), zaidi ya watu 200 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku zaidi ya watu 80 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Aidha, kisa cha kifo cha mtu mmoja kiliripotiwa nchini Uganda, hali inayoongeza umuhimu wa nchi jirani na wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari mapema.
Akizungumza kuhusu ugonjwa huo, Dkt. Hingora amesema Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Ebola (Ebola Virus Disease – EVD), ambao unaweza kuenea kwa kasi ikiwa hatua za kinga hazitazingatiwa.
Ugonjwa huo huathiri binadamu pamoja na baadhi ya wanyama wa porini, hususan nyani, sokwe na popo wanaodhaniwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya virusi hivyo.
Amefafanua kuwa Ebola huenea kupitia kugusana moja kwa moja na damu, mate, jasho, matapishi, mkojo au majimaji mengine ya mwili wa mtu aliyeambukizwa au aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.
Pia maambukizi yanaweza kutokea kwa kugusa vitu vilivyochafuliwa na majimaji hayo kama vile nguo, mashuka, vifaa tiba au kushiriki mazishi yasiyo salama ya mtu aliyefariki kwa Ebola.
DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA.
Dkt. Hingora amesema , dalili za Ebola zinaweza kuanza kujitokeza ndani ya siku 2 hadi 21 tangu mtu aambukizwe. Dalili za awali zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya kawaida, jambo linaloweza kufanya ugonjwa huo kutotambulika mapema.
Dalili hizo ni pamoja na:
Homa kali ya ghafla
Maumivu makali ya kichwa
Uchovu mkubwa na udhaifu wa mwili
Maumivu ya misuli na viungo
Koo kuuma
Kutapika na kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya kula
Katika hatua za baadaye, mgonjwa anaweza kupata dalili kali zaidi ikiwa ni pamoja na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili kama puani, mdomoni, machoni au kwenye haja kubwa, ingawa si wagonjwa wote hupata dalili hiyo.
Dkt. Hingora amesisitiza kuwa mtu yeyote mwenye dalili zinazofanana na Ebola, hasa aliyesafiri au kukutana na mtu kutoka eneo lenye mlipuko wa ugonjwa huo, anapaswa kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu badala ya kujitibu nyumbani.
JINSI YA KUJIKINGA NA EBOLA
Dkt. Hingora amewataka wananchi kuzingatia hatua zifuatazo za kinga ili kujilinda dhidi ya Ebola:
Kuepuka kugusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili wa mtu mwenye dalili za Ebola.
Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizer).
Kuepuka kushika au kula nyama za wanyama waliokufa porini bila uhakika wa usalama wake.
Kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu mazishi salama.
Kuripoti mapema kwa wahudumu wa afya endapo kuna mtu mwenye dalili zinazotiliwa shaka.
Kuepuka uvumi na kufuata taarifa rasmi kutoka Wizara ya Afya na wataalamu wa afya.
Aidha, amewahimiza wananchi kutokuwa na hofu kupita kiasi bali kuwa makini, kupata taarifa sahihi na kuchukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka za afya ili kuzuia ugonjwa huo kuingia na kuenea nchini.
“Kinga ni jukumu la kila mmoja wetu. Ni muhimu wananchi wakafuata maelekezo ya wataalamu wa afya na kuripoti mapema dalili zozote zinazotia shaka ili kulinda afya ya jamii,” amesema Dkt. Hingora.
Wizara ya Afya imeendelea kufuatilia kwa karibu mwenendo wa ugonjwa huo katika nchi jirani na kushirikiana na wadau mbalimbali wa afya kuhakikisha hatua stahiki za ufuatiliaji na udhibiti zinaendelea kuchukuliwa kwa usalama wa wananchi.
Elimu hiyo inakuja kufuatia taarifa za mlipuko wa ugonjwa wa Ebola katika maeneo mbalimbali ya barani Afrika, ambapo kwa mujibu wa taarifa za Kituo cha Udhibiti Magonjwa Afrika (Africa CDC), zaidi ya watu 200 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku zaidi ya watu 80 wakifariki dunia kutokana na ugonjwa huo.
Aidha, kisa cha kifo cha mtu mmoja kiliripotiwa nchini Uganda, hali inayoongeza umuhimu wa nchi jirani na wananchi kuwa makini na kuchukua tahadhari mapema.
Akizungumza kuhusu ugonjwa huo, Dkt. Hingora amesema Ebola ni ugonjwa hatari unaosababishwa na virusi vya Ebola (Ebola Virus Disease – EVD), ambao unaweza kuenea kwa kasi ikiwa hatua za kinga hazitazingatiwa.
Ugonjwa huo huathiri binadamu pamoja na baadhi ya wanyama wa porini, hususan nyani, sokwe na popo wanaodhaniwa kuwa miongoni mwa vyanzo vya virusi hivyo.
Amefafanua kuwa Ebola huenea kupitia kugusana moja kwa moja na damu, mate, jasho, matapishi, mkojo au majimaji mengine ya mwili wa mtu aliyeambukizwa au aliyefariki kutokana na ugonjwa huo.
Pia maambukizi yanaweza kutokea kwa kugusa vitu vilivyochafuliwa na majimaji hayo kama vile nguo, mashuka, vifaa tiba au kushiriki mazishi yasiyo salama ya mtu aliyefariki kwa Ebola.
DALILI ZA UGONJWA WA EBOLA.
Dkt. Hingora amesema , dalili za Ebola zinaweza kuanza kujitokeza ndani ya siku 2 hadi 21 tangu mtu aambukizwe. Dalili za awali zinaweza kufanana na magonjwa mengine ya kawaida, jambo linaloweza kufanya ugonjwa huo kutotambulika mapema.
Dalili hizo ni pamoja na:
Homa kali ya ghafla
Maumivu makali ya kichwa
Uchovu mkubwa na udhaifu wa mwili
Maumivu ya misuli na viungo
Koo kuuma
Kutapika na kuharisha
Maumivu ya tumbo
Kukosa hamu ya kula
Katika hatua za baadaye, mgonjwa anaweza kupata dalili kali zaidi ikiwa ni pamoja na kutokwa damu sehemu mbalimbali za mwili kama puani, mdomoni, machoni au kwenye haja kubwa, ingawa si wagonjwa wote hupata dalili hiyo.Dkt. Hingora amesisitiza kuwa mtu yeyote mwenye dalili zinazofanana na Ebola, hasa aliyesafiri au kukutana na mtu kutoka eneo lenye mlipuko wa ugonjwa huo, anapaswa kuwahi kituo cha afya kwa uchunguzi na matibabu badala ya kujitibu nyumbani.
JINSI YA KUJIKINGA NA EBOLA
Dkt. Hingora amewataka wananchi kuzingatia hatua zifuatazo za kinga ili kujilinda dhidi ya Ebola:
Kuepuka kugusana moja kwa moja na damu au majimaji ya mwili wa mtu mwenye dalili za Ebola.
Kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni au kutumia vitakasa mikono (sanitizer).Kuepuka kushika au kula nyama za wanyama waliokufa porini bila uhakika wa usalama wake.
Kufuata maelekezo ya wataalamu wa afya kuhusu mazishi salama.Kuripoti mapema kwa wahudumu wa afya endapo kuna mtu mwenye dalili zinazotiliwa shaka.
Kuepuka uvumi na kufuata taarifa rasmi kutoka Wizara ya Afya na wataalamu wa afya.Aidha, amewahimiza wananchi kutokuwa na hofu kupita kiasi bali kuwa makini, kupata taarifa sahihi na kuchukua tahadhari zinazotolewa na mamlaka za afya ili kuzuia ugonjwa huo kuingia na kuenea nchini.

Post a Comment