Serikali imesema hali ya ulinzi na usalama katika mipaka yote ya Tanzania yenye urefu wa kilomita 5,923.41 inayohusisha nchi kavu, anga na maji inaendelea kuwa shwari, huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kuchukua hatua madhubuti kuhakikisha mipaka hiyo inalindwa ipasavyo.
Hayo yameelezwa Mei 19, 2026 bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Dkt. Rhimo Nyansaho, wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Dkt. Nyansaho amesema licha ya kutokuwepo matukio yaliyoashiria uvunjifu wa amani kati ya Tanzania na nchi jirani, bado kuna changamoto mbalimbali zinazohitaji kuendelea kushughulikiwa ikiwemo uharibifu wa alama za mipaka, ubovu wa barabara za ulinzi na migogoro ya ndani katika baadhi ya nchi jirani.













Post a Comment