MAGEUZI YA ELIMU KWA MAENDELEO YA TAIFA -PRO MKENDA

..............

NA Ester Maile Dodoma 

Mageuzi ya elimu nchini hayaishii kwenye sera na mitaala pekee bali yanahusisha maeneo mbalimbali muhimu yanayolenga kuboresha sekta hiyo ikiwemo Sheria Miundombinu na Ubora wa Walimu.

Akiongea Mei 21, 2026 Jijini Dodoma wakati wa ufunguzi wa kikao cha wadau wa sekta ya elimu kilichokuwa kinajadili mapitio ya Sheria ya Elimu,Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda 

Amesema kuwa Serikali imekuwa ikijikita katika maeneo saba muhimu ambayo ni sera, sheria, mitaala, idadi ya walimu, ubora wa walimu, miundombinu pamoja na vitendea kazi.

Aidha, amebainisha kuwa sera ndiyo msingi mkuu unaotoa mwelekeo wa utekelezaji wa mambo yote katika sekta ya elimu huku sheria zikihitajika ili kuweka misingi ya utekelezaji wa sera hizo.

Ameongeza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya elimu kuanzia shule za awali hadi vyuo vikuu pamoja na kuhakikisha vitendea kazi kama vitabu vinapatikana vya kutosha




 

0/Post a Comment/Comments