MGOMBEA UBUNGE ISIMANI KUPITIA CCM AENDELEA KUGUSA MIOYO YA WANANCHI KWA AHADI ZA MAENDELEO


********

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Isimani kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM),Emmanuela Mtatifikolo, ameendelea kufanya kampeni zake katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo, huku akiendelea kuwahamasisha wananchi na kueleza dira yake ya maendeleo kwa Jimbo la Isimani.

Katika mwendelezo wa kampeni hizo, mgombea huyo ametembelea Kata ya Izazi pamoja na vijiji vyake na eneo la Malawi, ambapo alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi na kuwasilisha ahadi zake muhimu zinazolenga kuboresha maisha yao.

Akihutubia wananchi, Emmanuela alisema kuwa moja ya vipaumbele vyake vikubwa ni kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ndani ya jimbo hilo ambapo alieleza kuwa atahakikisha kunakuwa na Ujenzi wa zahanati ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi, Ujenzi wa skimu ya umwagiliaji ya Mkombozi kutoka Pawaga kwenda Makuka, hatua itakayosaidia wakulima wa mpunga kupata maji ya uhakika mashambani.

Ameongeza kuwa kuwa atakamilisha ujenzi wa barabara ya Makuka hadi kijiji cha Mnadani ili kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa Jimbo la Isimani.

Aidha, mgombea huyo aliahidi kushughulikia changamoto za huduma muhimu kwa wananchi kwa kuhakikisha,Mtandao wa maji katika kitongoji cha Makuka B unakamilika,Umeme wa REA unasambazwa katika vitongoji vyote ambavyo bado havijafikiwa na huduma hiyo muhimu.

Akihitimisha mkutano wake wa kampeni katani humo, Emmanuela aliwaomba wananchi wa Isimani kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi utakaofanyika mwezi Juni mwaka huu na kumpa kura za kishindo ili aweze kuwaletea maendeleo ya kweli na yenye manufaa kwa jamii nzima ya Isimani.













0/Post a Comment/Comments