MWILI WA MKAZI WA TEMEKE WAOKOTWA SALENDER


 *******

Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam limethibitisha kupokea taarifa ya kifo cha mwanamke aliyefahamika kwa jina la Aisha Miraji, mkazi wa Nzasa Temeke.

Mwili wa marehemu ulipatikana ukiwa kwenye maji eneo la daraja la Salender, Ilala, Mei 11, 2026 majira ya saa 4:30 asubuhi.

Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya polisi, mwili huo haukuonekana kuwa na jeraha lolote la wazi.

Polisi wamesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa Aisha alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Muhimbili Mei 10, 2026 akiwa pamoja na wazazi wake kabla ya kupotea ghafla hospitalini hapo.

Wazazi wa marehemu wameeleza kuwa mtoto wao alikuwa akisumbuliwa na changamoto za kiafya kwa nyakati tofauti ndani ya kipindi cha miaka mitano iliyopita.

Baada ya kupotea akiwa Muhimbili, juhudi za kumtafuta zilianza mara moja hadi mwili wake ulipopatikana eneo la Salender siku iliyofuata.

Jeshi la Polisi limesema linaendelea na uchunguzi wa kina kubaini mazingira halisi yaliyopelekea kifo hicho.


0/Post a Comment/Comments