******
SEKTA ya usafiri wa mtandao nchini imeendelea kukua kwa kasi huku Serikali ikisema huduma hizo sasa ni kichocheo muhimu cha uchumi wa kidijitali, ajira na kurahisisha usafiri kwa wananchi mijini,Takwimu zinaonyesha idadi ya madereva imeongezeka kutoka 943 mwaka 2021 hadi 11,946 mwaka 2024/2025.
Akizungumza katika kongamano la usafiri wa mtandao jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Msaidizi wa Huduma za Usafiri Sehemu ya Barabara, Andrew Magombano amesema Serikali itaendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji na sheria za sekta hiyo.
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Bolt Tanzania, Dimmy Kinyankole amesema kampuni hiyo inaendelea kuwekeza kwenye magari ya CNG pamoja na kupanua huduma zake katika miji mingine saba.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Chama cha Madereva wa Taxi Mtandao Tanzania (TODA), Ebony Ford amesema sekta hiyo imeendelea kuongeza kipato kwa madereva wengi nchini huku akisisitiza umuhimu wa kuboresha usalama na mifumo ya usimamizi wa huduma hizo.

Post a Comment