Tanzania imeendelea kuchukua hatua za kudhibiti ujenzi holela pembezoni mwa miji ili kuepuka gharama kubwa za kurekebisha miundombinu baadaye. Akizungumza katika Jukwaa la 13 la Miji Duniani (WUF13) jijini , Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, amesema serikali imeweka mkakati madhubuti wa kupanga ukuaji wa miji kabla makazi holela hayajashamiri.
Prof. Shemdoe amesema miji ya Dar es Salaam ,Mwanza ,Dodoma,Mbeya na Arusha inaendelea kukua kwa kasi hivyo mipango ya mapema ni muhimu ili kuepuka changamoto za makazi yasiyo rasmi, ukosefu wa ajira na huduma muhimu kama maji, umeme na usafi wa mazingira,Serikali pia imeanzisha matumizi ya mifumo ya kidijitali na GIS kurasimisha makazi na kupanga matumizi bora ya ardhi.
Aidha, serikali inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo Programu ya TACTIC katika miji 45 pamoja na Mradi wa Maendeleo ya Jiji la Dar es Salaam (DMDP) ili kuboresha barabara, masoko na kudhibiti mafuriko,Serikali pia imewekeza katika ujenzi wa masoko ya kisasa, vituo vya usindikaji mazao na Ukanda wa Kiuchumi wa Kwala kwa lengo la kuongeza ajira, kuimarisha uchumi wa miji na kupunguza msongamano wa maendeleo holela.








Post a Comment