TANZANIA NA UTURUKI ZAIMARISHA USHIRIKIANO KATIKA SEKTA ZA BIASHARA, UCHUMI NA UWEKEZAJI

*******

Serikali ya  Tanzania na ya Uturuki zimehitimisha mkutano wa kwanza wa ushirikiano jijini Dar es Salaam kuanzia Mei 4 hadi 5, ukiwa na lengo la kuimarisha mahusiano ya kiuchumi, biashara na uwekezaji kati ya nchi hizo mbili.

 Mkutano huo umejikita katika kujenga msingi imara wa ushirikiano wa muda mrefu unaolenga kuongeza fursa za kibiashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.

Akizungumza wakati wa kufunga mkutano huo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa, amesema majadiliano yamegusa sekta muhimu za kiuchumi ikiwemo biashara, uwekezaji, miundombinu na fedha. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa.

Ameeleza kuwa tayari pande hizo zimesaini makubaliano ya kuepuka kodi mara mbili, hatua inayotarajiwa kurahisisha mazingira ya uwekezaji na kuongeza mtiririko wa mitaji kati ya Tanzania na
 Uturuki. 
Katika hatua nyingine, Tanzania imeendelea kuwakaribisha wawekezaji kutoka Uturuki kuwekeza katika sekta za kimkakati kama viwanda, kilimo, utalii na miundombinu, huku ikilenga kuongeza thamani ya uzalishaji na ushindani wa bidhaa katika masoko ya kimataifa,aidha, nchi hiyo imekubali kuwa mwenyeji wa mkutano wa tatu wa Tume ya Pamoja ya Biashara, wakati mkutano wa pili ukitarajiwa kufanyika mwaka 2027 mjini Ankara, Uturuki, hatua itakayoongeza majadiliano ya fursa za kiuchumi na uwekezaji.
Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Volkan Işıkçı.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki, Volkan Işıkçı, ( hili jina la mwisho linatamkwa ISHIKISHE )amesisitiza dhamira ya nchi yake kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na Tanzania kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara, uwekezaji, afya, elimu na miundombinu,amesema ushirikiano huo utafungua fursa mpya za maendeleo na kuongeza manufaa ya kiuchumi kwa pande zote mbili. 





................MWISHO..........

0/Post a Comment/Comments