******
Serikali za Tanzania na Uturuki zimesaini mkataba muhimu wa kuondoa utozaji wa kodi mara mbili kwa bidhaa pamoja na kuzuia ukwepaji wa kodi ya mapato.
Makubaliano hayo yanatarajiwa kuboresha mazingira ya uwekezaji kati ya nchi hizo mbili na kuongeza ushirikiano wa kiuchumi.
Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar.Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utiaji saini, Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar, alisema hatua hiyo ni utekelezaji wa makubaliano ya mwaka 2011 ya kulinda na kukuza uchumi wa pande zote.
Alisema mkataba huo utaondoa changamoto ya kampuni kutozwa kodi mara mbili kwa kipato kilekile, hali ambayo imekuwa ikikwamisha uwekezaji.
Balozi Omar alieleza kuwa makubaliano hayo yataongeza tija kwa kampuni za Uturuki zinazoshiriki katika miradi ya kimkakati nchini, ikiwemo reli ya kisasa (SGR) na sekta ya viwanda.
Aidha, alisema hata kampuni za Tanzania zilizoekeza nchini Uturuki zitanufaika na mazingira bora ya kikodi.
Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Bekir Gezer.Kwa upande wake, Balozi wa Uturuki nchini Tanzania, Dkt. Bekir Gezer, alisema mkataba huo utaimarisha zaidi ushirikiano wa kidiplomasia na kiuchumi kati ya mataifa hayo mawili.
Alibainisha kuwa hatua hiyo ni ishara ya dhamira ya dhati ya kuendeleza uhusiano wa muda mrefu wenye manufaa kwa pande zote.

.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
.jpg)
Post a Comment