TMA YATOA MWELEKEO MSIMU WA KIPUPWE 2026

................

Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imesema katika msimu wa Kipupwe mwaka 2026 unatarajiwa kutawaliwa na hali ya baridi ya wastani hadi joto kiasi katika maeneo mengi ya nchi.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) na Makamu Mwenyekiti wa Jopo la Kimataifa la Sayansi ya Mabadiliko ya Hali ya Hewa na Tabianchi (IPCC) wakati akitoa mwelekeo wa hali ya hewa katika kipindi cha Mwezi Juni hadi Agost 2026 (JJA) .

Dkt Chang’a amesema kuwa katika kipindi hicho hali ya baridi ya wastani hadi Joto kiasi inatarajiwa katika maeneo ya Kanda ya Ziwa Victoria ,Kanda ya Magharibi,Kanda ya Kusini,Nyanda za Juu Kusini-Magharibi pamoja na Singida

Aidha Dkt Chang’a amesema kuwa maeneo ya ukanda wa pwani ikiwemo Dar es Salaam, Tanga, Pwani, Lindi na Mtwara yanatarajiwa kuwa na hali ya joto kiasi hadi baridi ya wastani, huku vipindi vya upepo mkali kutoka kusini vikitarajiwa kujitokeza zaidi katika miezi ya Juni na Julai.

Kuhusu Athari zinazoweza kujitokeza katika kipindi hicho TMA imesema magonjwa yanayohusiana na hali ya hewa ya baridi kama vile homa ya Mapafu na magonjwa ya mifugo yanaweza kujitokeza.

Dkt chan’ga amesema mwelekeo wa hali ya hewa kwa msimu wa Kipupwe (JJA) 2026, joto la bahari katika ukanda wa tropiki ya Bahari ya Pasifiki linatarajiwa kuwa juu ya wastani, jambo linaloashiria kujijenga kwa hali ya El Niño ambayo huathiri mifumo ya hali ya hewa duniani







 

0/Post a Comment/Comments