WAANDISHI WA HABARI WAPATA AJALI SHINYANGA,MMOJA AFARIKI

......

Gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari katika msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mboni Mhita, limepata ajali huku mmoja akifariki dunia na majeruhi watano wakipatiwa matibabu hospitali ya Rufaa ya mkoa huo.

 ‎ ‎Ajali hiyo imetokea jana majira kati ya saa 12 jioni Kata ya Usanda wilayani Shinyanga  wakati Mkuu huyo wa Mkoa akitokea Tinde wilayani humo katika ziara yake ya kufuatilia zoezi la utoaji wa huduma  wa msaada wa kisheria ya Mama Samia Legal Aid. ‎ ‎

Mmoja wa madereva katika msafara huo (jina limehifadhiwa) alisema wakati wakirudi Shinyanga mjini na walipofika Usanda ndipo wakakutana na Gari aina ya Harriew ikiwa mwendokasi na baada ya kuona msafara dereve alipoanza kupunguza mwendo ndipo ikamshinda na hatimaye kugongana na gari la waandishi wa habari. ‎

 ‎Alieleza kuwa gari hilo la waandishi wa habari lilikwenda kutumbukia kwenye kolongo na waliporudi kufanya maokozi waliwakuta wengine wametupwa pembezoni na baadhi kuning'inia kwenye milango akiwamo Mwandishi wa Habari wa ITV Frank Mshana. ‎ ‎

Aidha, baada ya taarifa zinadai majeruhi wanapatiwa matubabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wakiwamo pia Askari wawili na Dereva, huku Afisa habari mmoja wa Mkuu wa Mkoa Boaz Martine akifariki dunia na kupelekwa katika chumba cha kuhifadhia maiti. ‎
 

0/Post a Comment/Comments