WAZIRI KAPINGA ASISITIZA KIWANDA TBPL KUJITANGAZA KUJIENDESHA KIBIASHARA

Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga akizungumza katika Hafla ya utiaji saini hati za makubaliano baina ya TBPL (Kampuni Tanzu NDC) na TFC,TFRA,TARI na TPHPA ambayo imefayika leo tar 30/5/2026 katika kiwanda cha Tanzania Biotech Products Limited (TBPL) kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (NDC) Dr Nicolaus Shombe akizungumza katika Hafla ya utiaji saini hati za makubaliano baina ya TBPL (Kampuni Tanzu NDC) na TFC,TFRA,TARI na TPHPA ambayo imefayika leo tar 30/5/2026 katika kiwanda chaTanzania Biotech Products Limited  kilichopo Kibaha Mkoa wa Pwani.
..........

Waziri wa Viwanda na Biashara Judith Kapinga  amemuelekeza Katibu Mkuu wa wizara hiyo kusimamia kikamilifu uzalishanji kiwanda cha kuzalisha viuatirifu Biotech Products Limited (TBPL) kilichopo Kibaha Mkoani Pwani ili kuongeza Masoko ya bidhaa zinazozalishwa kiwandani hapo ndani na nje ya nchi

Waziri Kapinga ameeleza hayo leo Kibaha Mkoani Pwani katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano baina ya kiwanda cha TBPL (Kampuni Tanzu NDC) na TFC,TFRA,TARI na TPHPA.

Waiziri Kapinga amesisitiza kiwanda hicho kuzingatia ufanisi katika kuhakisha kinaendeshwa kibiashara zaidi kwani uzalishaji wa mbolea hai ni tija muhimu katika kuimarisha sekta ya kilimo.

Awali akizungumza Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (NDC) Dr Nicolaus Shombe amesema kuwa kwa sasa hali ya kiwanda hicho inaendelea kuimarika kwa kiasi kikubwa ambapo kwa mwaka 2025/2026 serikali imeweza kuuza dawa ndani na nje ya nchi.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbolea (TFC) Samweli Mshote amesema ushirikiano huo utakwenda kusaidia kukuza sekta ya mbolea nchini na kuongeza tija katika kilimo 
.
Naye Mkurugenzi wa TARI Dr Thomas Bwana ameeleza kuwa lengo lao ni kuendelea kufanya utafiti na kuzalisha teknolojia ambazo zinatatua changamoto za wakulima na mazao mengine ikiwemo udongo,mimea.

Akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Pwani,Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Nickson John amesema mkoa wa huo umeongeza viwanda kutoka 1387 mpaka 1722 huku Balozi wa Cuban nchini Tanzania Yordenis Vera akieleza kiwanda hicho anakiona kama ni alama ya uhusiano imara kati ya mataifa hayo mawili 

Katika Hafla hiyo wamehudhuria wiongozi mbalimbali wakiwemo Makatibu wa wizara ya Viwanda na Biashara,Mkuu wa Mkoa wa Pwani,wawakilishi kutoka wizara ya TAMISEMI,Afya,Kilimo na wananchi kwa ujumla. 
 











0/Post a Comment/Comments