Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU)
Mkoa wa Kinondoni kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni
imefanikiwa kudhibiti upotevu wa mapato zaidi ya shilingi Milioni mia tano
kutoka kwa wafanyabiashara wasiolipa ushuru wa huduma.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati akitoa
taarifa ya kipindi cha mwezi Januari hadi Machi 2026, Naibu Mkuu wa TAKUKURU
Mkoa Kinondoni Elizabeth Mokiwa amesema udhibiti huo umetokana na kupata
taarifa ya kuwepo baadhi ya wafanyabiashara hao kulingana na mauzo yao ya mwaka
kwa mujibu wa sheria.
Mokiwa amesema kuwa kitendo cha kukwepa kulipa ushuru husababisha upotevu wa mapato yanayostahili kukusanywa na Halmashauri hiyo kutofikia malengo ya makusanyo yaliyotarajiwa.
Aidha Takukuru Mkoa Kinondoni imefuatilia matumizi ya fedha za utekelezaji wa miradi ya maendeleo saba huku mitatu ikiwa sekta ya afya na minne ikiwa katika sekta ya elimu.
"Miradi mitatu ya sekta ya afya yenye thamani ya shilingi 1,625,960,706 ni pamoja na ujenzi wa jengo la ghorofa lenye wodi ya wazazi na sehemu ya upasuaji katika Zahanati ya Ndumbwi, jengo la magonjwa ya kuambukiza katika Hospitali ya Wilaya ya Kinondoni iliyopo Mabwepande pamoja na ujenzi wa uzio wa hospitali hiyo"amesema Mokiwa
Naibu Mkuu wa TAKUKURU Kinondoni amesema katika kipindi hicho pia yamepokelewa malalamiko 78 ambapo 26 yalihusu rushwa na mengine 52 hayakuhusu rushwa.
Katika hatua nyingine Taasisi hiyo imeendelea kuwasisitiza
wananchi kutoa taarifa za wapi alipo Alex Msama endapo watambaini kwenye maeneo
yao huku ikiahidi kutoa kitita kinono
cha pesa kwa atakayelifanikisha hilo.
xxxxxxxxxxxxxxx
Post a Comment