BARRICK YAWEZESHA KONGAMANO LA AIESEC ZANZIBAR


Mkuu wa wilaya ya Kati Zanzibar Rajab Ali Rajab akiongea katika kongamano hilo
Afisa Rasilimali Watu Mwandamizi wa Barrick Pius Kitunda akiongea na Wanafunzi na washiriki katika kongamano hilo.
Mkuu wa wilaya ya Kati Zanzibar Rajab Ali Rajab akibadilisha mawazo na Afisa Raslimali Watu Mwandamizi wa Barrick Pius Kitunda wakati wa kongamano hilo
Wageni meza kuu
  Wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu Zanzibar wameipongeza kampuni ya Barrick nchini na wadau mbalimbali kwa kudhamini kongamano la wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu ili ya kuwajengea uwezo wa kujiamini na kutambua fursa mbalimbali za kimaisha.

Kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, limeandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) na kufanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Zanzibar (SUZA).

Wakiongea kwa nyakati tofauti mwishoni mwa wiki wakati wa kongamano la hilo, lililofanyika Zanzibar baadhi ya wanafunzi walisema wameweza kujifunza mengi kupitia kongamano hilo sambamba na kujua shughuli za taasisi mbalimbali kubwa nchini na jinsi ya kutafuta fursa za ajira kwenye taasisi hizo ikiwemo jinsi ya kujiajiri baada ya kumaliza masomo yao.

"Makongamano kama haya ni moja ya njia ya kujifunza kwa kuwa kuna mambo mengi yanaendelea wanafunzi tunakuwa hatuyafahamu zaidi ya kufuatilia masomo tunayofundishwa darasani", alisema Khamis Ally Khamisi, Mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu cha Zanzibar akiongea kwa niaba ya wenzake.

Kupitia kongamano hilo ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao na jinsi ya kupata fursa za ajira kwenye makampuni mbalimbali.

Baadhi ya wafanyakazi wa Barrick nchini waliobobea katika fani mbalimbali pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.

Kongamano hilo lilihudhuriwa na wahadhiri kutoka vyuo mbalimbali ikiwemo viongozi wanaosimamia sekta ya elimu Zanzibar na mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Kati Zanzibar, Rajab Ali Rajab.
Mkuu wa wilaya ya Kati Zanzibar Rajab Ali Rajab akiongea katika kongamano hilo

0/Post a Comment/Comments