Bodi ya Filamu Tanzania imeahidi kuendelea kushirikiana na wadau mbalimbali kutoa nje ya nchi ya China ili kuongeza chachu ya suala la utamaduni wa filamu na masuala ya kijamii na kimaadili.
Kauli hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Dkt Gervas Kasiga wakati akizungumza kwenye Sherehe za Tamasha kubwa la watu wa china Dragon Boat festival ambalo limefanyika katika Kituo cha Utamaduni wa Kichina Upanga ambapo Mgeni rasmi amekuwa Balozi wa China nchini Tanzania Chen Mingjian.
Dkt Kasiga amesema kuwa bodi ya filamu imekuwa ni sehemu ya sherehe hizo kwani zinawakutanisha watu pamoja jambo linalosaidia kuongeza watalii wengi kuja kutembelea nchini ya Tanzania.
Aidha amesema ushirikiano huo ni matunda ya mshikamano uliojengwa na Viongozi wa kitaifa wa nchi zote mbili hivyo amewasisitiza watayarishaji wa filamu nchini Tanznaia kutumia fursa za matamasha mbalimbali pindi zinapojitokeza.
“Sisi kama Bodi ya Filamu Tumekuja hapa kuhakikisha tunaendelea kudumisha suala la amani na mshikamano lakini pia kuvutia watalii vivutia mbalimbali vya Tanzania ikiwemo Hifadhi ya Serengeti,Mlima Kilimanjaro,Hifadhi ya Ngorongoro,Visiwa vya Zanzibar na Kadhalika”amesema Dkt Kasiga
Katibu huyo wa Bodi ya Filamu amempongezeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluh Hassan kwa kujenga Diplomasia njema kwa watu wa China kupitia Rais wao jambo ambalo linasaidia kufanya shughuli zao za filamu kwa ufanisi.
Amesema kuwa kupitia mchezo wa filamu wanaousimamia wataendelea kuongeza fursa mbalimbali zikiwemo za matamasha ambayo yanaweza kuitangaza nchi kwa kuwa moja ya kituo muhimu cha kutayarisha filamu kwa ajili ya maendeleo
Kwa upande wake Balozi Chen Mingjian kuwa kufanyika kwa tamasha hilo nchini Tanzania ni ishara ya kuimarisha urafiki, mshikamano na maelewano kati ya wananchi wa Tanzania na China.
Hata hivyo ametumia fursa hiyo kuwasisitiza kufika katika Bodi hiyo na kujisajili wapate ithibati itakayofanya serikali iweze kupata idadi yao ili nafasi zinapojitokeza waweze kunufaika nazo.
Katika Tamasha hilo wamehudhuria akiwemo Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma kwa Wachina waishio Ng'ambo (Chinese Overseas Service Center), Bw. Zhu Jinfeng Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Tanzania, Michel Toto,





Post a Comment