DMI IMEWATAKA VIJANA KUSOMA KOZI ZINAZOENDANA NA SOKO LA AJIRA

.........

NA Ester Maile Dodoma 

Vijana wa Tanzania wametakiwa kutumia fursa zinazotolewa na taasisi za elimu ya bahari nchini ili kujijengea uwezo na kuongeza nafasi za kupata ajira ndani na nje ya nchi kupitia sekta ya usafirishaji wa majini na uchumi wa buluu.

Wito huo umetolewa na Muhadhiri Msaidizi katika Idara ya Uhandisi wa Meli ya Dar es Salaam Maritime Institute (DMI), Mhandisi Eng. Daniel Sylvester Nkipatala, ambaye amesema mafunzo yanayotolewa na chuo hicho yameendelea kuwawezesha wahitimu kupata ajira katika mashirika ya ndani na ya kimataifa pamoja na meli zinazofanya kazi nje ya Tanzania.

Amesema sekta ya maritime bado ina mahitaji makubwa ya wataalamu wenye ujuzi, hivyo vijana wanapaswa kuwekeza katika elimu na mafunzo ya fani za bahari ili kunufaika na fursa zilizopo katika soko la ajira la kimataifa.

Mhandisi Nkipatala pia amesema DMI huandaa Kongamano la Uchumi wa Buluu kila mwaka kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kwa lengo la kuhamasisha matumizi endelevu ya rasilimali za bahari na uhifadhi wa mazingira ya baharini.

Aidha, amesema taasisi hiyo inaendelea kutoa elimu kuhusu mazingira ya bahari kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla ili kuongeza uelewa na kuimarisha ushiriki katika shughuli za uhifadhi wa mazingira na maendeleo ya Uchumi wa Buluu nchini.





 

0/Post a Comment/Comments