KAMANDA MKONDA AWAPONGEZA ASKARI 06 WALIOFANYA VIZURI ZAIDI KATIKA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI

........

Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) William Mkonda amewapongeza Mkaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali 06 waliofanya vizuri zaidi katika utendaji kazi za Polisi Kikosi cha usalama barabarani Tanzania. 

Pongezi hizo zimetolewa leo Juni 05, 2026 katika viwanja vya Makao Makuu ya Kikosi cha Usalama Barabarani Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kumwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Camillus Wambura ambaye ametambua mchango wa askari hao katika kazi za Polisi.

Aidha, Kamanda Mkonda amewataka Maofisa, Wakaguzi na Askari wa vyeo mbalimbali kuendelea kutekeleza majukumu yao ya kusimamia sheria za usalama barabarani kwa kuzingatia umoja, nidhamu na weledi mkubwa ili kuhakikisha watumiaji wote wa barabara wanakuwa salama muda wote.





 

0/Post a Comment/Comments