MARIAM DITOPILE ASHIRIKI MBIO ZA MWENGE WA UHURU KONDOA MJINI


 ****

Mbunge wa Jimbo la Kondoa Mjini, *Mhe. Mariam Ditopile*, leo ameungana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama na wananchi kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Mji wa Kondoa, Mkoani Dodoma.

Mhe. Ditopile alishiriki shughuli mbalimbali za Mwenge wa Uhuru ikiwemo kukagua, kuzindua na kutembelea miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha huduma kwa wananchi katika sekta mbalimbali. Ushiriki wake umeonyesha dhamira ya kuendelea kusimamia na kuhamasisha maendeleo ya Jimbo la Kondoa Mjini sambamba na kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo endelevu.

Wakizungumza wakati wa shughuli hizo, wananchi walieleza kufurahishwa na ushiriki wa mbunge wao katika matukio muhimu ya maendeleo, wakisema uwepo wake unaimarisha mshikamano kati ya viongozi na wananchi katika kutekeleza agenda ya maendeleo ya jimbo hilo.

Baada ya mbio za Mwenge wa Uhuru, wananchi wa Kondoa Mji wanatarajiwa kushiriki mkesha mkubwa wa Mwenge wa Uhuru utakaofanyika katika Viwanja vya Sabasaba, ambapo wasanii mbalimbali watatoa burudani katika tamasha maalum lijulikanalo kama "Swahili Night". Mkesha huo unatarajiwa kuvutia mamia ya wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya Kondoa na wilaya jirani.

Mwenge wa Uhuru umeendelea kuwa chombo muhimu cha kuhamasisha uzalendo, umoja wa kitaifa na ushiriki wa wananchi katika shughuli za maendeleo, huku ukitumia fursa hiyo kukagua na kuhamasisha utekelezaji wa miradi yenye tija kwa jamii.










0/Post a Comment/Comments