Waziri wa Uchukuzi Profesa Makame Mnyaa Mbarawa, Juni 18, 2026, ametembelea eneo la upakiaji makontena na mizigo la ( Rail Terminal) lilipo Malindi Bandari ya Dar es Salaam
Lengo likiwa ni kukagua na kujiridhisha hatua iliyofikiwa ya kuanza kutoa huduma za usafirishaji wa mizigo kutoka Bandari ya Dar es salaam kuelekea vituo vya Morogoro, Ihumwa na Bahi, Mkoani Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kupunguza foleni ndani ya Bandari, Jiji la Dar es salaam na Barabara unganishi ya Dar es salaam hadi Morogoro.
Aidha hatua hiyo inatarajiwa kuwezesha uchukuzi wa mizigo mingi na mikubwa kwa wakati mmoja, kuelekea Mikoa mingine nchini na nje ya Nchi.
Uchukuzi wa Mizigo kwa kutumia reli ya Kisasa ya Standard Gauge Railway (SGR) ulianza Rasmi Mwezi Agosti 2025 kwa kuanzia eneo la Pugu, kwa hiyo kukamilika kwa eneo hili la Malindi litaongeza ufanisi wa Uchukuzi wa Mizigo.





Post a Comment