MKUTANO WA KIMATAIFA WA WATAALAMU WA SARATANI YA MFUMO WA FAHAMU KUFANYIKA TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akitoa taarifa mbele ya wanahabari jijini Dar es salaam leo tar 29,2026 kuhusu kufanyika mkutano huo Julai 13 hadi 15 mwaka huu 

......................

Wataalamu wa Saratani ya Mfumo wa Fahamu na wa afya kutoka nchi mbalimbali za Kusini mwa Jangwa la Sahara pamoja na mabara mengine duniani wanatarajia kukutana katika Mkutano wa Kimataifa nchini Tanzania ili kujadili changamoto zinazoikabili huduma za saratani ya mfumo wa fahamu ikiwemo upungufu wa wataalamu na vifaaa vya kisasa vya uchunguzi na matibabu.

Hayo yameelezwa jijini Dar es salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI), Balozi Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati akitoa taarifa ya kufanyika mkutano huo Julai 13 hadi 15 mwaka huu ambao umeandaliwa na Chama cha Wataalamu wa Saratani ya Mfumo wa Fahamu katika Ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa ushirikiano na Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) pamoja na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Balozi Dkt Ulisubisya amesema kuwa mkutano huo ni wa aina yake kwani nchini Tanzania na Kusini mwa Jangwa la Sahara kuna changamoto ya upungufu wa vifaa vya kiasasa vya kushughulika na magonjwa ya mfumo wa fahamu.  

Aidha amesema mkutano huo utatoa fursa ya kujadili mbinu za kisasa za kugundua mapema magonjwa ya mfumo wa fahamu, matumizi ya teknolojia za kisasa katika uchunguzi wa radiolojia, pamoja na matibabu sahihi na ya wakati. 

Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Radiolojia na Mwakilishi wa Chama cha Madaktari Bingwa wa Radiolojia Tanzania (TARASO), Dkt. Lulu Fundikira pamoja na Dkt Hamis Shaban Daktari bingwa wa Upasaji wa Magonjwa ya Ubongo,Uti wa Mgongo na Mishipa ya fahamu  MOI , amesema kuwa mkutano huo utakuwa ni fursa muhimu ya kueleza kazi wanazozifanya kutokana na kuongezeka kwa vifaa vya kisasa vya uchunguzi nchini jambo linalosaidia wagonjwa kupata matibabu kwa haraka.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Mkutano Dkt. Ugumba Kwikima amesema amesema Tanzania imepewa heshima ya kuwa mwenyeji wa mkutano huo kutokana na uwekezaji mkubwa unaoendelea kufanywa na Serikali katika kuimarisha huduma za afya kupitia upatikanaji wa vifaa vya kisasa kama Cath Lab, MRI na CT Scan, pamoja na kuongezeka kwa wataalamu wa uchunguzi, upimaji na matibabu wanaoshirikiana kwa karibu na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI) Dkt. Stephen Meena wamewasisitiza watadau mbalimbali kujumuika katika mkutano huo kwani utakuwa ni jukwaa muhimu la kubadilishana maarifa sambamba na kuimarisha ushirikiano kati ya wataalamu wa afya.

Mkutano huo utawaleta pamoja wataalamu wa afya kutoka mataifa mbalimbali ambapo pia utajadili kuhusu utoaji wa huduma za uchunguzi,matibabu na utafiti wa magonjwa hayo.














0/Post a Comment/Comments