SERIKALI YAIMARISHA USIMAMIZI WA UAGIZAJI MAFUTA KUPUNGUZA GHARAMA ZA DEMURAGE.

.........

Serikali imeendelea kuimarisha usimamizi wa uagizaji wa mafuta nchini kwa kuhakikisha meli zinazoleta mafuta zinapofika bandarini zinashusha shehena zake kwa wakati, hatua inayolenga kupunguza au kuondoa kabisa malipo ya kusubiri meli (demurrage).

Hayo yameelezwa na Mkaguzi wa Mafuta, ISSA Mwitazy, (PBPA) wakati akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea banda la sekta hiyo katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Chinangali jijini Dodoma.

Mwitazy amesema kuwa kupitia mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja, serikali imeweka utaratibu madhubuti wa kuratibu upokeaji wa mafuta ili kuhakikisha meli zinahudumiwa mara tu zinapowasili bandarini.

Amesema kuchelewa kushusha mafuta husababisha gharama za ziada ambazo zinaweza kuongeza bei ya bidhaa hiyo kwa watumiaji. Hata hivyo, juhudi zinazofanywa na serikali zimekuwa zikisaidia kuongeza ufanisi katika mnyororo wa ugavi wa mafuta nchini.

Aidha, Mwitazy amesema mfumo wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja umechangia kuhakikisha upatikanaji wa mafuta nchini, kuimarisha uwazi katika sekta ya mafuta na kuongeza ufanisi katika usimamizi wa bidhaa za mafuta.

Amesisitiza kuwa serikali itaendelea kuboresha mifumo ya usimamizi wa mafuta ili kuhakikisha huduma hiyo muhimu inapatikana kwa wakati na kwa gharama nafuu kwa wananchi.

Mwitazy amesema kuhusu mfumo wa SCADA umechangia kwa kiasi kikubwa kudhibiti upotevu wa mafuta ambao kwa muda mrefu ulikuwa changamoto.

Mfumo huu huungamisha kiwango Cha Mafuta kilichopokelewa kutoka melini na kiwango kilichofika kwenye maghala ambapo taarifa hutolewa mara moja endapo kutabainika tofauti yoyote ili hatua zichululiwa "Ameongeza Mwitazy 

"



 

0/Post a Comment/Comments