UDOM YAMUALIKA KAFULILA MHADHARA MAALUM KUHUSU NAFASI YA UBIA DIRA YA TAIFA 2050

******

Mkurugenzi Mtendaji wa Public Private Partnership Centre, Mhe. David Kafulila, anatarajiwa kutoa Mhadhara Maalum wa Umma Chuo Kikuu cha Dodoma (DODOMA UNIVNIVERSITY - UDOM) Juni 3, 2026, ukijikita katika nafasi ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) katika kuharakisha maendeleo ya Tanzania kuelekea Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.

Mhadhara huo, ulioandaliwa na College of Business and Economics (CoBE) kwa kushirikiana na PPP Centre, utajadili namna PPP inavyoweza kubadili miundombinu na utoaji wa huduma za umma sambamba, na kuchangia utekelezaji wa Mpango wa Tatu wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano.

Washiriki watapata fursa ya kujifunza kwa kina kuhusu mwelekeo wa maendeleo nchini Tanzania, nafasi ya sekta binafsi katika kuchochea ukuaji wa uchumi, pamoja na kushiriki majadiliano ya moja kwa moja na wataalamu wa sera na maendeleo.

Mhadhara huo utafanyika katika ukumbi wa CBSL_CT 1, CoBE–UDOM kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana, ukiwakutanisha wanafunzi, wahadhiri, watafiti, viongozi wa umma, wadau wa sekta binafsi na wananchi kwa ujumla.

"Jifunze. Jadili. Changia Maendeleo ya Tanzania kuelekea Dira 2050."

0/Post a Comment/Comments