WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) umehimiza wanawake wanaojihusisha na fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati (STEM) kulinda bunifu zao kupitia mfumo wa Miliki Ubunifu, ukieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kuongeza thamani ya ubunifu, kuibua fursa za biashara na kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa, amesema hayo wakati akifungua warsha ya Miliki Ubunifu kwa wanawake wa STEM jijini Dar es Salaam, akibainisha kuwa taasisi hiyo inaendelea na mkakati wa kuwafikia wabunifu wa kada mbalimbali ili kuwajengea uwezo wa kulinda na kurasimisha bunifu zao, hatua itakayosaidia kuyafanya mawazo ya
kibunifu kuwa fursa za kiuchumi. Cue In: Godfrey Nyaisa – Afisa Mtendaji Mkuu, BRELA.
Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Miliki Ubunifu wa BRELA, Bw. Seka Kasera, amesema kuongezeka kwa ushiriki wa wanawake katika fani za Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati kunatoa fursa kubwa ya kuibua ubunifu unaoweza kutatua changamoto za jamii, huku akieleza kuwa warsha hiyo inalenga kuwahamasisha wanawake hao kulinda na kunufaika na kazi zao.
Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wameeleza kuwa mafunzo hayo yamewapa uelewa kuhusu umuhimu wa kusajili na kulinda bunifu zao, wakisema hatua hiyo itawasaidia kuzuia wizi wa mawazo na kuongeza thamani ya kazi zao, ili ziweze kuchangia maendeleo ya jamii na taifa.






Post a Comment