.....
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mapema leo 9 Juni, 2026 Bi. Catalina Joseph (Mzazi) amemtembelea mwanae mwenye ujuzi wa kushona katika banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) na kushangazwa na kiwango kikubwa cha ubunifu na umahiri alioonyesha katika kazi zake.
Akizungumza baada ya kujionea bidhaa mbalimbali zilizoshonwa na mwanae, Bi. Catalina ameeleza kuwa hakuwa akidhania kama mafunzo hayo ya amali yangeleta mabadiliko ya haraka na makubwa kiasi hicho katika maisha na ujuzi wa mtoto wake.
Pia ameipongeza Mamlaka hiyo kwa kuweka mazingira wezeshi yanayosaidia vijana kujifunza kwa vitendo na hatimaye kujitegemea kiuchumi kupitia sanaa ya ushonaji.
Banda la Mamlaka ya Elimu Tanzania limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni wengi wanaotembelea maonesho hayo.


Post a Comment