BALOZI MULAMULA AKABIDHIWA TUZO YA UONGOZI BORA WA BODI YA WADHAMINI WA BENJAMINI MKAPA FOUNDATION

******

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya Benjamin Mkapa, Balozi Liberata Mulamula amepokea Tuzo ya uongozi bora wa Bodi hiyo, aliyokabidhiwa na Makamu wa Rais Balozi, Dk.Emmanuel Nchimbi kwa niaba ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.

Tuzo hiyo ilitolewa Jijini Dar es Salaam katika 

Jukwaa la Nne la Kuuenzi Urithi wa Hayati Rais Benjamin William Mkapa na Maadhimisho ya Miaka 20 ya Taasisi ya Benjamin William Mkapa Foundation katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC), Dar es Salaam.

Awali akizungumza, Mwenyekiti wa Bodi, Balozi Mulamula aliwashukuru viongozi na wadau mbalimbali waliojitokeza katika jukwa hilo muhimu la kuuenzi urithi wa Rais Benjamin Mkapa, huku akiahidi kuendelea kushirikiana na viongozi wengine wa Taasisi hiyo kutimiza malengo kusudiwa.

Pia, aliishukuru serikali ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan na ile ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Hussein Ali Mwinyi kwa dhamira yao ya dhati ya kuendeleza na kutambua mchango na urithi muhimu uliotolewa na Rais Mkapa.

Kwa upande wake, Rais Dk.Mwinyi, alisema njia bora ya kuuenzi urithi wa Hayati Benjamin William Mkapa ni kuendelea kuwekeza katika uongozi wenye maadili, kuimarisha mifumo ya afya na kuwawezesha vijana kuwa chachu ya maendeleo na wasanifu wa mustakabali wa Afrika.

Akitoa hotuba kwa niaba ya Rais Dk.Samia, Makamu wa Rais, Balozi Dk.Emmanuel Nchimbi, alisema serikali inathamini na kutambua mchango wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati Mkapa, katika kuendeleza afya bora ya Maendeleo ya Taifa, kupitia program mbalimbali na kumkumbuka kwa juhudi za mapambano ya magonjwa dhidi ya magonjwa yasiyo ambukiza na ya kuambukiza kwani alianzisha Time ya kudhibiti Ukimwi (TACAIDS).

0000


 

0/Post a Comment/Comments