NA HERI SHAABAN (ILALA)
MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, ametoa agizo kwa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam itenge bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya nishati safi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, alitoa agizo hilo Wilayani Ilala Mkoa Dar es Salaam, katika kikao kazi kilichowakutanisha Wakuu wa shule za Sekondari na wadau wa Mazingira.
"Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam mikakati yake imejipanga kuhakikisha ifikapo mwaka 2030 kila eneo linalohudumia watu 100 linatumia nishati safi naelekeza Halmashauri kutenga bajeti kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya nishati safi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali "amesema Mpogolo.
Mpogolo amesema dira ya Taifa ya matumizi ya nishati safi ifikapo mwaka 2050 Ilala inaendelea kuunga mkono Kampeni ya Kitaifa ya matumizi ya nishati safi inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan .
Aidha amesema Dkt.Samia Suluhu Hassan Kampeni yake ya nishati safi ya kupikia katika shule,masoko, na maeneo mbalimbali ya huduma za kijamii.
Ameeema matumizi ya nishati safi siyo uchaguzi bali ni wajibu wetu tuanze na shule,masoko na Taasisi zinazohudumia watu wengi ili kulinda mazingira na kuboresha afya za wananchi.
Mpogolo amesema katika wilaya ya Ilala shule kumi tayari zimeanza kutumia nishati safi na zingine tayari mikakati ya kuanza kutumia.



Post a Comment