DC MPOGOLO : ILALA IMETENGA FEDHA KWA AJILI YA CHANGAMOTO MACHINJIONI

.......

Na Heri Shaaban (Dar es Salaam)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo , amesema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imetenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa eneo maalum la mapokezi ya mbuzi machinjio ya kisasa Vingunguti wilayani Ilala. 

Akizungumza Dar es Salaam leo,wakati wa ziara Waziri wa mifugo na Uvuvi Balozi Dkt Bashiru Ally,.Mpogolo amesema dhumuni la kununua eneo hilo maalum kwa ajili kutatua changamoto za mbuzi kuzagaa eneo la machinjioni.

"Halmashauri yetu ya jiji la Dar es Salaam inatarajia kujenga eneo maalum la mapokezi ya mbuzi machinjio ya kisaaa Vingunguti hatua hii inalenga kumaliza changamoto ya mbuzi kuzagaa katika maeneo ya wazi wakati wakisubiri kuingizwa machinjioni"amesema Mpogolo. 

Mpogolo amesema eneo hilo likikamilika litaboresha usimamizi wa mifugo na mazingira ya machinjio ya kisaaa Vingunguti. 

Aidha amesema Serikali itaendelea kuboresha machinjio ya kisaaa Vingunguti ikiwemo kutatua changamoto za harufu kali ambayo wananchi walikuwa wakilalamikia kwa muda mrefu na wafanyabishara pamoja na wananchi. 

"Halmashauri tayari imenunua mtambo wa kuchakata mabaki kama ya mbolea hatua inayotarajiwa kupunguza uchafuzi wa Mazingira na kuongeza tija katika matumizi ya mabaki hayo.

Mwisho


 

0/Post a Comment/Comments