DC MPOGOLO: MIKAKATI YA ILALA NI KUSIMAMIA UFAULU

.............

 Na HeriShaaban(DaresSalaam)

MKUU wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo, amesema mikakati ya wilaya Ilala imesimama katika misingi ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere,pamoja ufaulu wa Wanafunzi kwa asilimia 100.

Mkuu wa Wilaya Mpogolo,amesema hayo wilayani Ilala Dar es Salaam, wakati kikao kazi cha idara ya Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam, ambapo pia kilitangaza matokeo ya mitihani ya ndani pamoja na kutoa tuzo kwa shule zilizofanya vizuri. 

"Ilala mikakati yetu kufaulisha wanafunzi kwa asilimia 100 pamoja na kusimamia Dira ya mwaka 2050 ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwani elimu ni bahari ambapo alitumia fursa hiyo kumpongeza Rais kwa kuajili walimu wapya 200 wa Sayansi na Hesabati pamoja na kuwekeza fedha nyingi za sekta ya Elimu zaidi ya bilioni 36 sasa hivi Ilala inaenda kujenga shule za kisasa za magorofa "amesema Mpogolo. 

Mpogolo aliwataka wajenge mahusiano wakasimamie misingi ya elimu sambamba na kwenda kusimamia ufaulu na kwenda kusimamia kituo cha Mitihani kilochopewa Jina la Edward Mpogolo kinachojengwa kwa fedha za Serikali shilingi milioni 432.

Aidha katika hatua nyingine amewataka wakajenge majengo ya TEHAMA kwa ajili ya Teknolojia ya kisasa pia alitumia fursa hiyo kumpongeza Afisa Elimu Sekondari Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Mwalimu Dkt.Mussa Ally kwa kufanya kazi kwa ushirikiano na Walimu wake pamoja na Baraza la Madiwani.

Mpogolo amesema Serikali ya awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaamini kuwa elimu ni uwekezaji wenye tija kwa maendeleo ya taifa, jambo linaloendana na utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 yenye lengo la kujenga taifa lenye wananchi wenye elimu, maarifa na ujuzi wa kushindana katika soko la dunia_.

_Akizungumzia siri ya mafanikio hayo. Mpogolo alisema, "Mafanikio haya yametokana na kuimarishwa kwa miundombinu ya shule, ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa elimu na wadau mbalimbali, pamoja na kuendelea kuboresha ubora wa ufundishaji na ujifunzaji_."

Mwisho





 

0/Post a Comment/Comments